• Breaking News

    HATUA ZA KUTHIBITISHA KUWA NI MTEULE WA MUNGU


    Bwana Yesu asifiwe ,

    Karibu katika kujifunza  Neno la Mungu, kwa MTEULE wa Mungu haiishii tu kwa Kumpokea Yesu kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako,Bali hatua za baada ya kumpokea Yesu kristo ni Muhmu sana ili kuthibitisha kuwa u Mteule wa Mungu, hatua ni nyingi chache katika hizo ni

    1.Kumtii Mungu katika mambo yote,                               Yakobo 4:8_10 "mkaribieni Mungu nae atawakaribia ninyi itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi, nakuidafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili,Huzunikeni na kuomboleza na  kulia, kucheka  kwenu kuwe kwa maombolezo na furaha yenu kuwa hama, jidhilini mbele za Bwana naye atawakuza

    2.Kuenenda katika Roho mtakatifu,
    Wagalatia 5:16_18" Enendeni kwa roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili,kwa sababu mwili hutamani ukishindana  na Roho na Roho kishindana na mwili kwa maaña hizi zote zimepingana,hata hamwezi kufanya anayotaka,lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria

    3.kujitenga na KILA dhambi za zamani yaani kabla ujaokoka  Zaburi 34:14 "Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifuate"


    4.kuendelea mbele katika imani ya wokovu wa Bwana Yesu Wakolosai 2:6_7 " Basi kama mlivyompokeaKristo Bwana basi Enendeni vivyo hivyokatika yeye  wenye shida na wenye kujengwa katika yeye mmefanywa  imara kwa imani kamamlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani

    5.Kumtumikia Bwana Yesu, 1Wakotinto 15:58" Basi ndugu zangu wapendwa mwimarike,msitikishike mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote kwakua mwajua kwamba taabu YENU si ya bure katika Bwana"   unajua kwamba kuna tofauti kati ya mwsnafunzi na mwamini, kuna tofauti ya mwsnafunzi wa kiroho na mwamini,   Mwanafunzi anamalengo ya kufikia mtu Fulani ,mwamini ni mwamini tu hubaki kuwa mwamini, Bali Mwanafunzi wa kiroho vanatoka katika kundi la waamini maaña wote walimwamini  Yesu kristo na kumpokea kama mwokozi ,Hapo ndipo imani utofautiana kati ya mteule  na mwingine,Mwanafunzi  haishi tu  kuwa Mwanafunzi,Bali  ujipambanua kuwa yeye ni Mwanafunzi wa Yesu anayejifunza sana ili ajue mambo mengi ya ki Mungu na ili baadaye akiwa katika nafasi fulani kiutumishi  atende vema na vizuri,sijui kama umenielewa ndugu lengo usiishie tu katika kuamini,Bali jifunze Biblia na uwe mwombaji na fanya kila Jambo  la ki Mungu ambalo waliofanikiwa kiroho wamefanya,wapo watu ili wafunge na kuomba mpaka watangaziwe madhabauni
    Imani utofautiana  baina ya Mtu na mtu kwa sababu ya
    1. Uelewa na uzingatiaji wa Neno la Mungu                    1 Petro 2:2" kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa,ilikwa moyo mpate kuukulia wokovu

    2. Imani huwa inamacho ya kuona hivyo Mungu ili imani yako iwe kubwa lazima uipalilie imani hiyo, 2wakorinto 5:7" maaña twaenenda kwa imani si kwa kuona"  unaipalilia kwa maombi ya Mara kwa mara,kujitskasa, kusoma neno na kuliamishia katika Matendo

    3 Kumtumikia Mungu                                                         1Wakorinto4:1" mtu atuhesabu ivi kuwa tu watumishi wa kristo na mawakili wa siri za Mungu"

    Hayo ndiyo wanaweza kumtofautisha mtu na mtu katika imani, kumbuka imani chanzo chake ni kusikia,hivyo kumbe unavyosikia Mara kwa mara ndivyo imani inavyojengeka, Je imani yako kama haisikii Neno la Mungu Mara kwa mara itajengwa katka nini? Je? Imani iyo itakuwezesha kuomba kwa Mungu ikakuleta majibu, la! Hapana, kumbe tunajifunza kunawatu wanaongezeka viwango vya imani na wengine la!
    Watu wengi hawawaxi ya Mungu wanawazaya duniani na mambo ya duniani upindisha fahamu za watu     1Yohana 2:15" Msipende DUNIA ,wala mambo yaliyo katika dunia,mtu akipenda dunia kumpenda Baba Mungu akupo ndani yake, ndugu akikisha unatumis muda wako kuwaza yaliyo yaMungu utafanikiwa,   Mithali 3:5_6" Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri yeye naye naye atayanyosha mapito yako, Ni muhimu sana kuwaza yaliyo ya MUNGU maaña tupo kipindicha Zama za uongo  Hata akili zako tu usizitegemee ,waza yaliyo ya Mungu , isiwaze yaliyo ya DUNIA ,Waza yaliyo ya MUNGU wala si ya dunia.
    Isaya 55:8" Maaña mawazo yangu si mawazo YENU wala njia zangu si njiaBwana
    ,asema Bwana

    Kuwaza yaliyo ya MUNGU ni
    1.Kuwaza Neno na kisha kuamua kulitii
    2 kuwaza MAOMBI na kisha kuamua kuwa mtu wa maombi
    3.Kuwaza ibada na kuamua kuwa mtu wa kuudhuria ibada
    4.kuwaza njia za Mungu za kufanikiwa kwako
    5.kuwaza wokovu wa kristo na kuchukua hatua za kuishi maisha ya wokovu
    6.Kumtafakari Bwana Yesu na kazi zake
    7.kumuwaza Roho Mtakatifu na kwa jinsi gani umtiidaima ili uumpendeze Mungu

    Mambo hayo ndiyo yanayowatofautisha wateule katika ukuwaji wao wa kiroho,  Waefeso 5:15_17" Basi angalieni jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na Hekima, Bali watu wenye Hekima, mkiukomboa wakati maaña Zama hizi ni Zama za uovu,kwa sababu iyo msiwe wajinga,Bali  mfahamu ni nini? yaliyo mapenzi ya Bwana
    Nmepewa nafasi ya kuomba lakini wewe uombi vikija vifungo vya kipepo utalalamika
    Umepewa nafasi ya kutumika na Bwana  lakini wewe utumiki,nafasi iyo ikiondolewa kwako utatumia nguvu nyingi kuirudisha nafasi iyo
    Umepewa nafasi ya kushuudia lakini haushuudii,na watu wanatakiwa kufikiwa na injili yako awapo duniani,Je utapata furaha gani, ndugu yangubnalkuomba uutumie nafasi vyema uliyopewa na Mungu katika injili ya Yesu kristo Mwokozi
    Unaitaji sana Neno  ili ukuwe kiroho na imani yako iongezeke
    Mungu amekuletea walimu wengi tu ili wakupe maarifa yatakayoinua Imani yako hivyobinakupasa kuzingatia fundisho la Neno laMungu
    Katika injili ya Yesu kristo kuna walimu wengi wa Neno la Mungu wengine wapole na wengine wakali,kuna walimu wenye Hekima sana na walimu wenye kujua Neno zaidi,kuna ambao wako vizuri sana katika kufundisha maombi,wengine siku zamwisho,wengine utoaji,wengine masomo Fulani nakadhalika lakini kuna vitu viwili ambavyo kila mwalimu amepewa kufundisha ni utakatifu na wokovu ,KILA mwalimu wa Neno la Mungu ni wa muhimu sana,ndugu usichague mwalimu wa kukufundisha Neno la Mungu labda tu walimu wa Biblia ambao wapo kinyume na Bibli au Neno  la Mungu
    Lakini kama yupo mwalimu wa Biblia au Neno la Mungu na anafundisha kwa usahii na kwa kusudi la Mungu, uyo mwalimu ruhusu moyo wako akufundishe Neno la Mungu ,haijarishi ninmwalimu mkali au anakemea Sana au mwalimu anayeyerudia rudia Neno ,Na mwalimu ninaye mzungumzia hapa si lazima aitwe mwalimu anaweza akawa mwinjilisti,mchungaji,mtume nabii aunmzee wa kanisan  yeyote yule anayefundisha Neno la Mungu basi msikilize na fanyia kazi Neno  ilo,kumbuka mteuliwa wa MUNGU aliyekombolewa  na Mungu anathibitishwa na vitu viwili

    1.Matendo yake 1Petro 2:11_12" wapenzi nawasihi kama wapitaji na wasafiri ,ziepukani tamaa zamwilizipiganazo na roho mwe na mwenendo mzuti kati ya Mataifa,ili iwapo  huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo Matendo YENU mazuri wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa"

    2.Maneno ya kinywa chake,    Wakolosai  3 9_10" msiambiane uongo kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale pamoja namatendo yake mkivaa utu mpya  upya unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeumba"
    Mteule wa Mungu lazima aya mawili yakuthibitishe
    Wakristo wengi vinywa vyao havikiri injili Bali vinakiri mambo ya dunia tu
    Wakristo wengi midomo yao imefunikwa siku zote, maaña awatangazi injili ya Kristo
    Hakika Matendo yako yanahubiri injiri ya Kristo, hakika kwa maneno ya kinywa chako na kwa Matendo yako yanahubiri   habari njema za ufalme wa Mungu katika  Kristo Yesu
    Matendo yako  ushuuda wa kukuonyesha wewe ni mtu wa aina gani,Matendo ni ushuuda mkubwa kuliko vyote
    Kataa dhambi,iache dhambi ,ikimbie dhambi na usifanye  dhambi tena
    Kitu kingine Muhmu sana ukuwe kiroho ni ibada katia ibada uwa kuna ,uponyaji, mda wa ibada kunaushindi wa kiroho ni muhimu sana KILA mmoja wetu kuwa mtu wa ibada ,Mungu anatafuta watu wamwabudu katika kweli yake
    Yohana 4:24 " Mungu ni Roho ,nao wamwabudio yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli,

    Natamani kusema mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa nmeelewa Mungu akubariki kwa kujifunza Neno ili lakini ninaneno la mwisho  kwako

    Bwana Yesu amekaribia kurudia
    Je umejiandaaje ,Je unaendelea na dhambi ili siku ile uachwe na Bwana  Yesu ,Je umeshika wokovu na utakatifuu ata siku ile unyakuliwe ukaishi maisha ya milele ?, majibu unayo moyoni mwako ,Nakusihi umpokee Yesu kuwa Bwana na mwokozi wake  na uishi maisha matakatifu ukiwa ndani ya wokovu, vya DUNIA tulivikuta na tutaviacha usipoteze mda wako ukasahau kuokoka ,vya duniani visikusahaulishe ata ukasahau wokovu wa Bwana wako Yesu
    Ni Mimi mtendakazi wako Peter M Mabula
    Pia masomo kama haya ya kila siku unaweza kupata katika blogi hi pia katika GodloveApp, unaweza ku download katika link(http://goo.gl/pRBmJp)











    No comments