• Breaking News

    ITA MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO

    Leo ngoja tuangalie somo letu nzuri la msaaada wakati wa magumu, kila mtu akipata tatizo huwa anaweza omba msaada Mahali fulani au kuitisha usaidizi Mahali fulani, hata jeshi au kikosi fulani Cha jeshi pindi kikiwa katika harakati za kutimiza wajibu wake kikishindwa huwa kinaweza omba msaada kutoka pengine au kikosi kingine,. Je sisi wakiristo tukipata shida tunaomba msaada kwa Nani, Watu wengi wakipata shida uenda kwa waganga, au wachawi wanaeleza shida zao,. Mkiristo unaomba msaada kutoka wapi. Mungu kwetu Ni msaada kwa sababu Biblia inatuambia kuwa Mungu kwetu Ni msaada tosha wa mwili na kiroho, kwa sababu

    1.Bwana ndiye Tumaini na ngome nyakati za shida, Tunasoma katika kitabu cha Zaburi 9:9_10, Bwana  hana desturi ya kumwacha mtu

    2.Mungu ukimlilia wakati wa shida anasikia, na hadharau teso la mteswa, hivyo Basi Ni  Bora kuita msaada wa Mungu wakati wa shida, zaburi 22:24

    3.Hata ndugu zako wa karibu wakikuacha Mungu hawezi kukuacha,tuna Tunasoma katika Zaburi 27:10_14, Mungu anasema waziwazi hato kuacha

    4.Bwana hushika mkono husianguke ijapo kuwa umejikwaa, Daudi anasema tangu ujana wake Hadi uzee hajawahi ona mwenye haki akiachwa Wala watoto wake wakiomba mikate barabarani, Zaburi 37:24_28,

    5.Bwana Hisikia na ujibu wakati ukimwita, Zaburi 18:1_9 inatueleza vizuri kuwa Mungu anajibu endapo utamlilia, na hata anaweza tikisa nchi kwa ili akujibu maombi yako

    6.Kwetu Ni kimbilio na nguvu, si kimbilio tu maaana makimbilio Ni mengi akaongezea na nguvu,👇

    7.ukimuita Mungu kwamwe hatasababisha huondoshwe kamwe na shida au tatizo, Zaburi 55:22 inatueleza zaidi

    8.Mungu hutupa nafasi ya kusimama,Hata unapokuwa taabuni, Zaburi 31:7

    9.Bwana huona ugumu na Mateso ya wanna wake,ata wana wa Israel waliokolewa Maana kilio Chao kilifika mbele za Bwana, kutoka 3:7

    10.Bwana atakulinda, atakufadhili atakufadhili, Tunasoma Katika kitabu cha Zaburi 41:1_5


    11.Mungu atakupa nafasi ya kusimama Tena, Mika  7:8_10

    12.Ijapo kuwa tunasongwa na dhiki hatutakata tamaa Maana Mungu ndiye kimbilio letu, 2Wakoritho 4:8_9



    Hazi Ni sababu ambazo Mkristo azifahamu kwa Nini anaitaji kumuita Mungu Wala si kitu au watu wengine wanapopita katika magumu
    Asante

    Usikose kutufuatilia katika masomo yetu katika blog Yetu pendwa Pia unaweza download application yetu kwenye linki Apo chini,Na pia unaweza wasiliana Nasi kwa namba 0755555070/0752390465 usisite kutoa maoni na ushauri
    Asante

    No comments