• Breaking News

    IkIWA UTALIAMINI NENO LA MUNGU KAMA LINAVYOSEMA YOTE YANAWEZEKANA

    Ukiwa utaliamini neno la Mungu kama linavyosema yote  yanawezekana  usipo Amini haiwezekani
    Mithali 30:5_6 " Kila Neno la Mungu limehakikishwa;Yeye ni ngao yao wamwaminio. 6 usiongeze neno katika maneno yake; usije akakulaumu, ukaonekana u mwongo"    Yeremia 1:12 "Ndipo Bwana akaniambia, umeona vema; kwa maaña ninaliangalia neno langu,ili nilitimize"
    Neno la Mungu limehakikishwa na analitazama alitimize, Zaburi 18:30" MUngu njia yake ni kamilifu  ahadi ya Bwana imehakikishwa  Yeye ndiye ngao yao wote wanaomkimbilia"     Efeso 3:20" Basi  atukuzwe awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuwezayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu"

    SHIDA NI NINI? _ kutokuamini sawasawa na neno linavyosema na kutoamini watumishi wa Mungu
    Mfano no 1. mfano wa Akida, Mathayo 8: 5_13 "Hata alipoingia kapernaumu, akida mmoja alimjia,. 6 akamsihi, akisema, Bwana, Bwana mtumish amelala nyumbani ,mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana, 7 Yesu Akamwambia, nitakuja nimponye. 8 Yule akida akajibu akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu;lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona, 9 Kwa maaña mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye Askari chini yangu;nikimwambia huyu,Nenda, huenda, na huyu njoo, huja na mtumwa wangu fanya hivi hufanya, 10 Yesu aliposikia hayo,alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata,Amini,nawaambieni, sijaona imani kubwa namna hii, kwa yeyote katika Israel, 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watatoka kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahim,na Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni, 12 Bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa na kilio na kusaga meno. 13 Na Yesu Akamwambia yule akida, n
    Nenda zako; na iwe  kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile"


    Mfano no 2.  Ushuuda wa Mama mlima na Mchungaji       palitokea mama mmoja katika kanisa fulani, Mama huyo alikuwa na shamba dogo sana ambalo limebanwa na kilima juu yake hivyo kusababisha kutoweza kulima kutokana na kuwa na mlima huo kulinganisha na majirani wenzake waliopakana naye. Kutokana na hivyo kila mwaka alilima eneo dogo hivyo kusababisha kutokuwa na chakula cha kutosha na Mama huyo alikuwa masikini na hana pesa ya kununua eneo lingine, siku moja kanisan mchungaji akamkaribisha mchungaji mwenzake ili afundishe semina, Mchungaji huyo alifundisha somo la imani na akasema  "Kwa Mungu yote yanawezekana kama ilivyo katika Biblia" na mwisho wa semina akasema mwenye shida aje mbele tuombe kwa Mungu juu ya shida yake,  Mama yule akaenda na kumwambia mchungaji yeye ombi lake ni Mlima uliyoko shambani kwake  uondoke, Lakini mchungaji Akamwambia Je  unamaanisha mlima wa kawaida au mlima tatizo, mama yule akasema mlima kama mlima upo shambani kwake na mchungaji umefundisha kuwa kwa Mungu yote yanawezekana, Watu pamoja na mchungaji wakaaza kucheka juu ya ombi lake na kuaza kuona mama yule analeta mambo ya ajabu lakini yeye akiomba aombewe juu ya ombi lake, Mchungaji alimwombea kwa shingo upande ombi lake, Walipokwisha kusali mchungaji wa semina ile Akamwambia mchungaji mwenyeji wako kuwa nimekutana na Mama ambaye anataka mlima utoke shambani mwake wote wakastahajabu.Mama yule aliendelea kuomba kila siku na Màombi yake bila kusita kwa kila ibada na kila màombi mpaka wakampatia jiñà la Mama mlima, siku zikapita njingi mama mlima aliendelea na Màombi mwishoni akasema unamwachia Mungu lakini kwake yeye yote yanawezekana.  Baada ya siku kazaa kupita kukatokea ujenzi wa barabara na wakandarasi wa maeneo yale walitafuta kifusi kizuri maeneo yale wakakikosa, baadaye wakakumbuka kuwa kunamlima sehemu unaweza kufaa kwa kifusi cha barabara lakini kunashamba la mtu ambaye ni yule mama ambaye alipewa jina la mama mlima, ndipo wale wakandarasi wakaamua kwenda kumuomba yule mama shamba lake ili wapate nafasi ya kuuondoa ule mlima katika shamba lake, Na yule mama akawaambia anachotaka mlima uondoke tu ndiyo haja yake. Wale wakandarasi wakampatia  Yule mama pesa nyingi sana kutokana na fidia ya shamba lake na mlima wake ulio katika shamba lake!!!! Hallelujah na toka siku ile mama yule  aliuaga umaskini na kutoa changamoto ata kwa mchungaji wake
    Kwahiyo Mtu wa Mungu Ikiwa utaliamini neno kama lisemavyo  Yote YANAWEZEKANA aijarishi ni changamoto ipi, aijarishi Nani kasema haiwezekani, Wewe simamia Neno la Mungu


    Mfano no 3. Naamani 2Wafalme 5:13_15" Watumish wake wakakaribia wakamwambia,Baba yangu,kama nabii angalikuambia kutenda Jambo kubwa, usingalitenda, Je si zaidi basi, akikwambia jioshe uwe safi?  Na ndipo akashuka akajichovya Mara Saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu, Nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga akawa safi, akamrudia yule mtu wa Mungu yeye na mafuatano yake,akasema sasa tazama najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote,la katika Israel, basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako
    Somo  hili  limeandaliwa na mchungaji kikoti ulanda, 0746314369, Pia masomo kama Haya yanapatikana  katika blog hii au GodloveApp unaweza kudownload katika link(http/goo.gl/pRBmJp) na pia unaweza tangaza Nasi kwa matangazo mbalimbali, contact 0712945827,Asante karibu

    1 comment:

    1. Asnte sana mtumishi kwa somo zuri ambalo nimelipata kupitia ukurasa wako.
      Kusema kweli siku zote nilikuwa nafunga lakini nilikuwa sijui maana ya kufunga , nadhani nilikuwa nafuatia mapokeo ya wazazi na dini lakini kila kukicha nazidi kujiuliza kwa nini nafnga nimesikia mafundisho mengi na mahali pengi lakini nikawa sielewi chochote ndipo siku moja nilisikia mafundisho ya kufunga kutoka kwa mtumishi wa Mungu, Mtume Bonifasi Mwamposa kuhusu kufunga ndipo nilipofumbuliwa macho maana ya kufunga na wakati naanza kufuatilia kufunga nikakutana na huu ukurasa nao pia umezidi kunipa matumaini makubwa kuhusu kufunga Mungu awabariki sana na awazidishie pale mlipotumika kuelimisha jamii kwa neno lake Amina.

      ReplyDelete