• Breaking News

    WAKATI WA MAJARIBU

    Wakati wa kujaribiwa mambo mengi huweza tokea katika kipindi hicho, Mkiristo wa kweli na mwenye imani katika Kristo lazima kwa namna moja au nyingine anaweza kuwa anapitia. Lakini katika hayo Kuna mambo ya msingi ambayo binadamu au Mkiristo anatakiwa kufahamu wakati wa kipindi hicho, Twende tuangalie vitu vya kukumbuka wakati wa majaribu ambavyo biblia inatuambia,

    1.Mungu Ni mwaminifu,hatakuacha, Lazima atafanya mlango wa kutokea,Na hamtajaribiwa kupita kiwango Cha kustahimili,   1Wakoritho:10:13

    2.Lazima mbele kunaushindi,Maana tunajuana hakika hakuna kitu kinachoweza kututenga na upendo wa Kristo, Warumi 8:37

    3.Yote magumu itafika wakati yataisha/ yataondoka kwako, na Mungu ndiye atakayeyaondoa, Muhubiri 7:18


    4.Mungu huwaondoa wenye haki wake katika majaribu,   2Petro 2:9


    5.Mjaribiwa pia lazima akumbuke kuwa Neema ya Mungu yatosha kufanya wokovu, 2Wakoritho 12:9

    6.Mungu husaidia watu kushinda Maana hata yeye mwenyewe alijaribiwa, waebrania 2:18

    7.Lazima ukumbuke Mungu Ni mkuu kuliko vyote hivyo ukiwa nae lazima ushinde 1Yohana:44

    8.Hata ivyo Mungu wakati wote atakutia moyo katika jaribu lako. Isaya 51:12

    9.Usitende dhambi, Katika majaribu Jambo la kukumbuka mkristo Ni kutotenda dhambi wakati wa majaribu, Ayubu alijaribiwa mpaka watu wa ji
    jirani kwake wakawa wanamshawishi Ayubu atende dhambi ili afe lakini Ayubu hata akiwa katika hali ya ngozi kuharibika Sana alisema, Pasipo mwili huu nitamwona Bwana, yani alijitoa kufa na kupona ilimradi asitende dhambi, Na Ayubu aligungua kabsa hata akifa katika hali hiyo Atamuona Mungu katika hali nyingine, Ayubu 19:26

    Hayo Ni baadhi ya vitu au mambo ya kukumbuka wakati unapitia mambo magumu mbalimbali katika maisha ambayo kwa ufupi tu nimekuletea upate kujifunza
    Asante

    Usikose kutufuatilia katika masomo yetu katika blog yetu, Pia unaweza download application yetu kwenye linki Apo chini au tunapatikana kwa namba 0755555070/0752390465 usikose kutoa maoni na ushauri wako

    No comments