Ndugu Mpendwa msomaji, leo nakuletea someone nzuri la Baraka za Mungu kwa wale WANAOMTUMIKIA, Somo Hili likujenge na kukujazia kuwa Mungu amesharuhusu Baraka zake tangu mwanzo kwa watu wake, Kuna Baraka nyingi Sana lakini ngoja tuziangalie Baraka chache tu ambazo zimeandikwa kwenye bibilia,
I.Utakuwa na chemichemi ya Uzima, na watu wa nyumba yako watashibishwa kwa unono, Zaburi 36:8_9
2.Mungu hubariki kwa kukufundisha namna ambayo utapata faida mara dufu, atazidisha uzao wako kama mchanga na Amani kama mto wa maji, katika maisha yako, Isaya 48:17_19
3.Bwana atabariki chakula chako, atakuondolea magonjwa, hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba,Wala tasa na Wala miaka ya siku zako za kuishi hazitakatishwa na kitu chochote kile, iwe ajali, magonjwa, shida Wala kitu chochote kile, Kutoka 23:25_27
4.Hutabarikiwa kwa kufurahia mema ambayo Bwana anakupa katika maisha yako, kumbukumbu la Torati 26:11,
5.Mungu hubariki kila mahali, Hubariki Mjini ata kijijini, hubariki uzao wako, mashamba yako, watoto wako, mifugo yako na kila Aina ya Baraka Kwa watu wake Mungu hubariki, Kumbukumbu la Torati 28:1_14, imeeleza Sana juu ya Baraka ikiwa utamtumikia Mungu
6. Mungu hubariki kwa kuwategemeza wenye haki,yeye kuwapa mahitaji yao, huwapa urithi wa milele, na hata wakati was ubaya hawataharibika kamwe
7.Baraka za Bwana si za huzuni, Wala si za manung'uniko Wal kuumiza Bali Ni Baraka za Furaha katika maisha na tena hutajirisha, Mithali 10:22
8.Mungu pia hubariki kwa making pasipo kuwa na taabu na hizo Mali, Mithali 15:16
9.Mungu hubariki kwa kukupa hekima na maarifa,Bali mkosaji humpa taabu, Myhubiri 2:24_26
10.Mungu humpa mtumishi wake maisha ya kitajiri, Muhubiri 5:19_20
11.Mungu hubariki hata kwa kukukarimu kwa karama sake upate Kula na kunywa
12.Mungu atabariki kizazi hata kizazi na kizazi Cha mwenye haki kitaokolewa, Pamoja na kurithi nchi, Mithali 11:22
Mithali 14:26
Mithali 20:7
Hizo Ni Baraka za Mungu kwa wale WANAOMTUMIKIA, nazo Ni chache ambazo tumezichambua lakini Mungu anabaraka nyingi na nzuri
Asante
Usikose kutufuatilia katika masomo yetu katika blog Yetu pendwa, Pia unaweza download application yetu ya Godloveapp kwa kubonyeza link Apo chini, pia tunapatikana kwa Namba 0755555070/0752390465, Kwa maoni na ushauri
No comments