Leo katika mwendeoezo wa masomo Yetu tunaangalia Namna Mungu Ambavyo hatuwezi kumficha katika kila Jambo ambalo tunafanya. Ingawa Kuna Wakristo wengi huwa ujificha katika kichaka Cha kufanya maovu na mara nyingi labda kuwaogopa watu wanaowazunguka na kusahau kuwa wanashuhudiwa na Mungu kwa kila Jambo wanalotenda, Ngoja tuangalie maandiko yanayotuthibitishia kuwa Ni vigumu kujificha mbele za Mungu
1.Zaburi 139:8_13, Biblia inatuonyesha hakuna mazingira ambayo binadamu anaweza kujiwekea au kujatafuta ili tu aepukane na Uwepo wa Mungu, Mungu yupo kila mahali
2.Yeremia 23:24, katika kitabu cha Yeremia Mungu anauliza Ni nani Ambaye atajificha hata asimuone, Mana yeye ndiye aliyevijaza vitu vyote
3.Ayubu 34:21_22, kitabu cha Ayubu kinatuelezea kuwa Mungu hafichwi na chochote kile wawezapo kujificha wanadamu wakifanya maovu
3.Mithali 15:3, Mithali inaeleza kuwa Mungu huwatazama watu wote Wema na wabaya katika Matendo yao
4.Luka 8:17,Mungu hafichwi at na neno ambalo hutamkwa kwa uwazi au usiri,
5.Matendo ya Mitume 17:27,Pia Maandiko hutuambia kuwa Mungu hayuko mbali na kila mtu, ivyo Ni vigumu kumficha kitu mbele yake
Aya Ni baadhi ya maandiko yanayotuthibitishia kuwa Mungu huwezi jificha mbele zake hata kidogo, Mpendwa Basi Sasa umejua kuwa Mungu hafichwi na kitu chochote Basi Ni Bora ukatubu ukawa salama, Maana Mungu husamee .
Asante
Usikose kutufuatilia katika masomo mbalimbali katika blog Yetu pendwa, Pia unaweza download application yetu kwenye linki Apo chini,Na unaweza kuwasiliana nasi kwa Namba 0755555070/0752390465, Pia usisite kutoa maoni yako Asante
No comments