• Breaking News

    FAHAMU MAOMBI YA KUFUNGA NA FAIDA ZAKE

    Tunaposema kuhusu maombi, maombi ni nini?_ maombi ni mawasiliano kati ya Mtu  na mtu au mtu na Mungu
    Kuna  aina mbili za màombi
    1.maombi ya kawaida
    2.maombi ya kufunga na kuomba

               MAOMBI YA KAWAIDA
    Haya ni màombi ambayo mtu anaweza kuyafanya bila kufunga, Haya uitwa màombi ya kawaida

              MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA
    Haya ni màombi ya kutoa gharama ili kufikia viwango vya hitaji. Si rahisi lazima ujitoe, kwanini? Kwa sababu  Yesu amesema mengine hayawezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba, Mathayo 17:21" Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga"

    SHIDA NI NINI?_ Huwezi kuwa na msukumo kama hujui faida zake,kutojua faida ni shida.  Isaya 58:1_30

             KWA NINI TUNATAKIWA KUFUNGA

    1.maombi ni uchaguzi wa Mungu wa kuzuia nguvu za giza na kazi zake,  Mathayo 6:13" Na usitutie majaribuni lakini utuokoe  na yule mwovu,kwakuwa ufalme ni wako,na nguvu na utukufu hata milele"  Efeso 6:12_18 "  kwa sababu hiyo twaeni siraha zote za Mungu mpate kuweza kushinda siku ya uovu, mkiisha kuyatimiza yote kusimama. 13  Basi simameni ,Hali mmejifunga kweli viunoni na kuvaa dirihi ya haki kifuani. 14 Na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa ajiri ya amani. 15 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizuia mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 16 Tena mpokee chepeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu. 17 kwa sala zote na màombi mkisali kila wakati katika  Roho mkikesha kwa Jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.18 pia kwa ajiri yangu Mimi,nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu ili nihubiri kwa ujasiri ile siri ya injiri.
    2.maombi hutupatia msaada wa Mungu kila wakati katika Hali zote , Zaburi 3:3_4  "Na wewe,Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu namwinua kichwa changu, 4 Kwa sauti yangu namwita Bwana, Naye aniitikia toka mlima wake Mtakatifu"   Zaburi 33:4_6 "Kwakuwa Neno la Bwana linaadili na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. 5 huzipenda haki na hukumu , Nchi imejaa fadhili za Bwana, 6 kwa  Neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.

    3 Màombi huondoa vikwazo au vipingamizi,  Marko  11:23_24  "Amini nawaambia,yeyote atakayruwambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini wala usione Shaka moyoni mwake ila aamini kwamba Haya asemayo yatakuwa yake,. 24 Na kwa sababu hiyo yeyeote myaombayo mkisali,Amini  ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu"⏩⏩

    4.maombi ni njia ya kupata amani tunapokabiliwa na hhila za kukatishwa tamaa,  Wafilipi 4:4_7"upole wenu na  ujulikane na watu wote,Bwana yu karibu, 5 msijisumbue kwa Neno lolote Bali katika kila Neno  kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru,haja zenu na zijulikane na Mungu, 6 Na amani ya MUNGU ,ipitayo  akili zote,hiwaifadhi  mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu, 7 Hatimaye ndugu zangu mambo yoyote yaliyo ya kweli, yaliyo ya staha ,yaliyo ya haki, yeyote yaliyo Safi, yeyote yenye sifa njema, ukiwepo
     wema wowote ikiwapo  sifa nzuri yeyote, yatafakarini hayo."

    5Màombi hugeuza mioyo yetu na watu wengine  Nehemia 2:4_8 na kuendelea, "4 Ndipo mfalme ananiambia una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni, 5 Nikamwambia mfalme, mfalme akiona vema na ikiwa Mimi,mtumishi wako nimepata kibali machoni pako,Tafadhali unipeleke mpaka Yuda, Niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, Nipate kuujenga, 6 Mfalme akaniuliza (malkia ameketi karibu naye) Safari yako Itakuwa siku ngapi? Nawe utarudi lini?, Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka,Nami nikamnga'mbo 7 Tena nikamwambia mfalme akiona vema na nipewe nyaraka kwa maliwali walio nga'mbo ya mto,ili nimuache mpaka nifike Yuda nipewe na waraka wa Asafu mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba  ile nitakayoingia Mimi,naye mfalme akanipa ,kama mkono mwema wa Mungu ulivyokuwa juu yangu," ⏩⏩

    6.Maombi ni njia ya uponyaji wa kimwili na kiroho   Yakobo 5:14_15  "Na  kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na Bwana atawinua hata ikiwa wamefanya  dhambi atasamehewa, 15 ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa, kuomba kwake mwenye haki kwafafa sana akiomba kwa bidii'

    7.Maombi huachilia msukumo wa Nguvu za kiroho katika utumishi,   Rumi 8:26_27 " Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho  ilivyo,kwa kuwa huwaombe watakatifu kama apendavyo Mungu, 27 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema Yaani wale wilioitwa kwa kusudi lake"

    👆👆Hizo ni sababu zinazotufanya kuwa  na maombi ya kufunga
    Usikose sehemu ya tatu ya somo hili,ambayo itazungumzia faida ya maombi ya kufunga
                                       Mungu akubariki
    Somo hili limeandaliwa na mchungaji kikoti ulanda, 0746314369, pia masomo Haya ya kila siku unaweza kuyapata katika blog hi au GodloveApp katika link(http:/goo.gl/pRBmJp)

    3 comments:

    1. Kwa kuongezea, unaweza kusoma hapa kujua faida nyingine za maombi...>>> https://wingulamashahidi.org/2019/08/04/faida-za-maombi/

      ReplyDelete
      Replies
      1. Shukran Sana wingu la mashaidi. Kama inawezekana tutaftane kwa simu 0755555070 whattsp

        Delete