• Breaking News

    TUNAPOKUMBUKA NA KUSHEHEREKEA KUFUFUKA KWA KRISTO KUTUKUMBUSHE NAMNA TUNAVYOISHI

    Maandiko, Mathayo 28:1_10 "Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya Juma Mariamu Magdalena,na Mariamu yule wa pili,walikwenda kulitazama kaburi. 2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akaliviringisha lile jiwe akalikalia. 3 Na surà yake ilikuwa kama umeme,na mavazi yake kama theluji. 4 Na kwa kumuogopa,wale walinzi wakatetemeka,wakawa kama wafu. 5 Malaika akajibu,akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi kwa maaña  najua mnamtafuta Yesu aliyesurubiwa. 6 Hayupo hapa; amefufuka kama alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipolazwa. 7 Nanyi Enendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona.Haya nimekwisha waambia. 8 wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. 9 Na tazama Yesu akakutana nao,akisema, Salamu! wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. 10 Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona."
    Pia katika Yohana 20:1_30, na kuendelea anazungumzia habari za kufufuka kwa Kristo

    Swali ni Je!?

    1.ushindi wa Kristo ulisehemu ya maisha yetu ya kila siku

    2.Tunamfanania kristo katika maisha yetu kwa maneno na tabia

    3.Tunawasamehe waliotukosea? Kama tulivyosamehewa, Mathayo 6:14_15"kwa maaña mkiwasamehe watu makosa yao,na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao,wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu"

    4.Tunahubiri injiri kwa Matendo Na maneno,  Mathayo 28:18_20" 18 Yesu akaja kwao, akisema nao,akawaambia,Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani 19 Basi, enendeni mkawafanye wataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na kwa Roho Mtakatifu; na kuyashika na kuwafundisha yote niliyowaamuru ninyi; na tazama mimi nipo pamoja Nanyi siku zote, hata  ukamilifu wa dahari."


                       TUFANYE NINI
    1.Tukumbuke kwa kumaanisha kutoka moyoni,Tupo wapi/Tumebadilika au

    2.Tunza  Matendo ya kwanza ,Upendo wa kwanza,  Ufunuo 2:4" lakini Nina neno juu yako kwamba umeuacha Upendo wako wa kwanza"    Ufunuo 2:24_26" 24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo wasiojua fumbo za shetani kama vile wasemavyo, sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25 ila mlichaonacho kishikeni sana,Hata nitakapokuja. 26 Na yeye ashindaye na kuyatunza Matendo yangu hata mwisho, Nitampa mamlaka juu ya mataifa"

    3.Ishi maisha ya kujikana hubiri injiri watu waokoke

    HALLELUJAH YESU KAFUFUKA HAYUPO TENA KABURINI


    Somo hili limeandaliwa na mchungaji kikoti ulanda 0746314369, katika semina  ya pasaka, Usikose sehemu ya pili ya katika blog hii au GodloveApp unaweza kudownload katika link(http:/goo.gl/pRBmJp)


    2 comments: