• Breaking News

    ROHO MTAKATIFU

    Roho Mtakatifu ni Nani? _ ili umjue Roho Mtakatifu lazima ujue Ni Nani
    Roho Mtakatifu ni Mungu, Matendo 5:3_5


    Ni mshiriki katika nafsi tatu za Mungu


                                                  Sifa za  Roho Mtakatifu
    1.Ana Asili ya umilele,. Walaka wa Ebrania 9:14



    2.Roho Mtakatifu yupo kila Mahali, kila wakati, Zaburi 139:7_8 inatueleza vizuri kuwa Roho Mtakatifu yupo kila mahali


    3.Roho Mtakatifu anafahamu yote , tunaona katika kitabu cha Wakoritho wa kwanza kuw Roho Mtakatifu  anajua yote 1Wakoritho 2:10-11

    4.Roho Mtakatifu anaweza yote ,Roho  Mtakatifu anaweza mambo yote, tunaona katika kitabu cha Luka kuwa Roho Mtakatifu anaweza kutanya mambo ambayo kibinadamu Ni magumu kabisa, Luka 1:35




    UWEZO ALIONAO

    1.Kuona moyoni, Riho Mtakatifu anauwezo wa kuona moyoni, mawazo na vitu vyote ambayo binadamu au kitu chochote au kiumbe kiwazayo, Efeso 4:30

    2.Roho Mtakatifu anauwezo wa kufariji, hili tunaakikishiwa na maandiko katika kitabu cha Matendo kuwa Roho Mtakatifu anaweza kufariji, Matendo 9:31


    3.Roho Mtakatifu anauwezo wa kuomba, ata hivyo Biblia inatuthibitishia kuwa Roho Mtakatifu anaweza kuomba katika kitabu cha Warumi, Warumi 8:25_26
    4.Roho Mtakatifu anaweza kufundisha, hili tunapata katika andik la Yohana kuwa Roho Mtakatifu pia anao uwezo wa kufundisha, Yohana 14:26

    5.Roho Mtakatifu anaweza kuzuia Jambo fulani lisitokee au anaouwezo wa kusababisha Jambo fulani kutokea , Matendo 16:6


    Haya Ni baadhi ya Mambo machache kuhusu Roho Mtakatifu, usichoke kufatilia blog yetu hi, kwa somo linalofuata la Roho Mtakatifu sehemu ya Pili

    No comments