• Breaking News

    Moyo Uliovunjika

    Moyo uliovunjika

    Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

    Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.”

    Lengo la semina ni kushughulika na waliovunjika moyo na wale ambao wako tayari kupona. Hata kama haujavunjika moyo, hebu chukua mafundisho haya kama chakula cha njiani kwani mafundisho haya sijayatoa kwasababu ninazo notisi tu bali ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, Mungu atawaponya wengi kwenye hii semina.
    Maana ya neno moyo linavyotumika kwenye Biblia:
    ü  Moyo ni kiungo kilichoko katika mwili kinachotumika kusukuma damu
    ü  Moyo imetafsiriwa kama nafsi
    ü  Moyo imetafsiriwa kama roho
    ü  Moyo ni utu wa ndani wa mtu (Nafsi +roho)
    ü  Moyo ni kiini cha uhai wa kitu
    Moyo uliovunjika ni wa namna gani? Ni moyo ulioharibika au kujeruhiwa baada ya kushindwa kubeba ilichokibeba. Moyo uliumbwa kwa ajili ya kumbeba Mungu moyoni. Mambo ambayo moyo hauwezi kuyabeba:

    1. Moyo hauwezi kubeba hasira au uchungu kwa zaidi ya masaa 12.
    Efeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

    2 Korinth 7:10 “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.”

    2. Moyo wa mwanadamu hautakiwi kubeba dhambi
    Ezekiel 18:4 “Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.”

    3. Moyo haukuumbiwa kubeba au kupigana vita
    1 samwel 31:3-4 “3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.”
    Vita ni vya Bwana na si vya mtu.

    4. Moyo haukuumbiwa kubeba lawama
    Zab 69:19-20 “19 Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. 20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.”

    5. Moyo haukuumbiwa njia ndefu, au kuzimia au kuchoka
    Hesabu 21:4-5 “4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. 5 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.”

    ·         Madhara ya moyo kuvunjika yanaweza kuonekana kwa:
    - moyo wa mtu mwenyewe
    - marafiki wa mtu aliyevunjika moyo

    Mithali 28:24 “Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.”

    ·         Kiongozi akijeruhiwa ni hatari.
    Matokeo yake yataonekana nje kwa wale anaowaongoza
    Nahumu 3:18-19 “18 Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya. 19 Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima?”
    Kukataliwa kunaumiza moyo sana.

    ·         Nchi inaweza kujeruhiwa na Jeraha inaweza kuwa kubwa
    Yere 30:4,12 “4 Na haya ndiyo maneno aliyosema Bwana, katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda.…… 12 Maana Bwana asema hivi, Maumivu yako hayaponyekani, na jeraha yako ni kubwa.
    Unaweza kupona jeraha juu juu tu. Kwa hiyo ni vizuri kuhakikisha kujua hilo jeraha limeponyeka lote au la.
    Yer 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”
    Na pia ni vizuri kujua na kushughulikia chanzo cha jeraha, na si tu mtu alitumiwa kuleta jeraha.



    Leo nakutangazia ya kwamba Mungu anaponya majeraha na kwenye neno hili utaposoma!


     

    No comments