• Breaking News

    ALIYEJAZWA ROHO MTAKATIFU

    Leo katika mwendelezo wa Masomo Yetu, Tutagusia tabia au ishara ya Mkiristo kuwa kajazwa na Roho Mtakatifu, Kama kawaida yetu huwa atujiongozi wenyewe Bali tunaongozwa na Maandiko katika bibilia Maana  ndiyo Mwongozo wetu wa kila siku, kwa kifupi tunaangalia maandiko katika bibilia, Tuazee

    1.Watu waliojazwa Roho Mtakatifu hawafwati mwili Bali wafata Roho, Hii Ni moja ya sifa ya watu waliojazwa Roho Mtakatifu, maisha yao hawafuati kwa namna ya Mwili, . Warumi 8:9

    2.Waliojazwa na Roho Mtakatifu huwa wema, wamejawa na imani, waongezekao upande wa Mungu, Matendo ya Mitume 11:24

    3.Hushika Neno la Bwana na sheria zake, Pamoja na kuzitenda. Si kuzishika sheria za Bwana hasha Bali  kuzitenda, Ezekieli 36:27

    4.Hunena kwa Lugha, watu waliojazwa Roho Mtakatifu hunena kwa Lugha kwa ujasiri, Matendo ya Mitume 4:31

    5.Wanakuwa na nguvu, na Mashaidi wa Roho Mtakatifu, Apo siyo nguvu ya kibinadamu Bali Ni nguvu za kiroho za kushinda uovu, kutangaza injili na kuzitenda kazi za Mungu, Matendo 1:8

    6:Huwa na vipawa, Kama ivivyoandikwa Roho Mtakatifu  ufanya wengine kuwa walimu, wengine wainjilisti, lakini pia Mungu huzidi kuwajaza Sana Roho Mtakatifu wale wamchao

    Hizo Ni baadhi ya Tabia na sifa za watu waliojazwa Roho Mtakatifu katika maisha yao, Na hizo bila kupunguka ata moja, yaan uwezi ukawa unanena kwa Lugha lakini ufati maagizo ya Bwana, hivyo Basi yote haya uambatana Pamoja

    Asante


    usikose kutufuatilia katika masomo yetu katika blog Yetu pendwa,Pia unaweza download application yetu kwenye linki Apo chini Na kuendelea kupata update zetu kila siku, Na  tunapatikana kwa namba 0755555070/0752390465, usikose kutoa maoni yako

                                                     ( htt/goo.gl/pRBmJp)




    No comments