• Breaking News

    KRISTO AJA MARA YA PILI

    Leo wapenzi wasomaji wa blog Yetu pendwa, Nawaletea somo Hili la kuja kwake Kristo Mara ya Pili, wapenzi wasomaji leo hii  Nawajuza na kuwakumbusha kuwa Kama Kristo alivyosema kuwa atarudi kuchukua kanisa basi Sasa Mimi na wewe ndio kanisa lenyewe, Swali Je tumejiandaa kwa kuja kwake, Wakristo wezangu Yesu atakaporudi atachukua kanisa ambalo ni Safi, kanisa Takatifu, kanisa ambalo halijabeba hata chembe ya Dhambi, Je sisi Ni miongoni mwa Hilo kanisa, Basi ngoja tuangalie maandiko yanayoelezea Naman Yesu Atakavyorudi

    1.Luka Mtakatifu 12:40, Yesu alikuwa akawaambia wanafunzi wake kuwa Ni lazima kujiwekea tayari Maana Saa wasiyodhani Mwana wa Adamu ajapo, labda tungeweza kusema saa ambayo binadamu hategemei ndiyo hiyo saa ambayo Yesu anaweza kurudi, labida niweke kwa Lugha nyepesi tuweze kuelewana na kuweza kulielewa somo, Wakati wa Nuhu wakati wakiendelea kuoana, wakati wakiendelea kucheza muziki, na kuabudu miungu mingine k kila haina ya uovu na kumsahau Mungua liye hai, na kujisahau kutubu ndipo Mungu akashusha gharika, Hatupo mbali kimtazamo na kizazi kile Cha Nuhu Mana hata leo hii watu wakiendelea busy na Kukaa mbali na Mungu,labda tungeweza kusema watu wakiendelea na uchawi,uongo, watu wakiendelea kwenda club kila siku, watu wakiendelea kufanya uzizi na maovu mengi na wakijisahau kuwa Yesu yu karibu kurudi.

    2.Luka Mtakatifu 21:27,Biblia inatuelezea kwa namna gan Yesu atakuja na nguvu Pamoja na Utukufu

    3.Yesu atakuja kulipa watu kwa kadri ya Matendo yao, Mathayo 16:27

    4.Mathayo 24:27 ,Biblia inasema Kama vile umeme namna ya ujio Wakristo Mara ya Pili

    5.Ufunuo wa Yohana 16:15, Biblia inatuambia kuwa Ni Kama mwivi namna itakavyokuwa,

    6.Waraka wa Kwanza was Yohane 3:2,

    Ndugu Mpendwa msomaji haya Ni baadhi ya maandiko yanayotuthibitishia kuwa Yesu atarudi Mara ya Pili na Je kwa ujio wake Yesu tutakuwa tumejiandaa,Basi Sasa Ni wakati wako wa kujiandaa kwa kutubu na kufanya mapezi yake Mungu
    Asante

    Basi usikose kutufuatilia katika masomo yetu katika blog Yetu pendwa, Pia unaweza download application yetu kwenye linki Apo chini, au Tutaweza wasiliana kwa namba 0755555070/0752390465. Asante

    (htt/goo.gl/pRBmJp) Godloveapp

    1 comment:

    1. God bless you servant of God and your family, marriage and even your jobšŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ’„šŸ”„

      ReplyDelete